Tanzania: Update kwa hali ya Mh. Tundu Lissu

By  |  0 Comments

Hali ya Tundu Lissu bado si ya kuridhisha, ameshafanyiwa oparesheni tatu, inaonesha alipigwa risasi zaidi ya tano
Kuanzia jana asubuhi, Lissu alianza kusikia maumivu ya kifua, mguu wake wa kulia umevunjwavunjwa kwa risasi.
Mguu wa kulia wa Lissu umevunjwavunjwa zaidi ya mara 3 au mara 5, nyonga na mkono vimevunjwa kwa risasi.
Amevunjwavunjwa pia mguu wa kushoto kwa risasi, amevunjwavunjwa nyonga na ameongezwa damu nyingi sana.
Jana hali yake ilibadilika na kuwa mbaya sana, akawa anapumua kwa mashine, madaktari wamefanya kazi kubwa, leo ameamka salama.
Kwa sasa madaktari wanahangaika kuunganisha mifupa yake iliyovunjwa kwa risasi, tutahakikisha tunafanya kila liwezekanalo apone.
Alivyoondoka Lissu hatujui kama atarudi vile alivyokuwa mwanzoni, lakini tutapokea atavyokuwa maana ni zawadi tuliyopewa na Mungu.
Dk. Vincent mashinji
Katibu mkuu CHADEMA.

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *