Tanzania: Rais Magufuli atoa tamko kuhusu tukio la Lissu

By  |  0 Comments

Rais John Magufuli amesikitishwa na taarifa alizozipata tukio la kupigwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa nyumbani kwake Dodoma leo na kuviagiza vyombo vya dola viwasake waliyofanya uhalifu huo.
Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter jioni ya leo na kutaka vyombo vya usalama kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo la kinyama.
“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hilo la kinyama na kuwafikisha katika mikono ya sheria”, ameandika Rais Magufuli.
Tundu Lissu amepigwa risasi leo mchana akiwa yupo nyumbani kwake mjini Dodoma ‘Area D’ kwa ajili ya kupata chakula cha mchana baada ya kutoka katika viwanja vya Bunge

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *