Tanzania: Lissu kuwahishwa Nairobi kwa matibabu

By  |  0 Comments

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Mbunge wa Singida Mashariki ambaye emepigwa risasi na watu wasiojulikana, ametoka chumba cha upasuaji na anatarajiwa kupelekwa Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara kupitia CHADEMA Mh. Joyce Sokombi ambaye yupo hospitali hapo, amesema kwa sasa Mh. Lissu ametolewa chumba cha upasuaji na anapumzishwa ili kuweza kumsafirisha kwenda Nairobi mara atakapopata fahamu.
“Lissu ameshatoka chumba cha upasuaji na wamempumzisha mpaka atakapoamka, wamsafirishe kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi, taarifa za matibabu yake zitatolewa na uongozi”, alisema Joyce Sokombi.
Tundu Lissu amepigwa risasi leo mchana majira ya saa 7:30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma, na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ili kunusuru maisha yake.

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *