Breaking News: Rais Nkurunziza atuma ujumbe kwa Magufuli eti warundi walio kimbia katika Nchi ya Tanzania warundi Nchini

By  |  0 Comments

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amemuomba Rais John Magufuli kuwasihi wananchi wake walio kimbia nchini humo kurejea, akimuhakikishia kua hali ni shwari.

Baadhi ya warundi walio kimbia Nnchi hiyowakihofia maisha yao kutokana na vurugu za kisiasa zilizo tokea wakati wa uchaguzi mkuu baada ya kupinga kiongozi huo kugombea tena.

Katika uchumbe uliowasilishwa ikulu jana na Mnadhimu wa jeshi la Burundi, Meja Jenerari Evariste Ndayishimiye, ambae ni mjumbe maalumu wa Rais Nkurunziza, kiongozi huyo alimuomba Rais Magufuli ambae ni mwenyeketi wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuwasihi wananchi wa Burundi walio kimbia nchi yao warejee nyumbani.

Meja Jenerarli Ndayishimiye Akimueleza Rais Magufuli kwamba ametumwa kuleta barua hiyo pamoja na shukrani za dhati kwa Tanzania ambao ni rafiki, jirani na ndugu wa kweli wa Burundi kwa mshirikiano mzuri inaoupata.

Dk John Pombe Magufuli alimshukuru Rais Nkurunziza kwa ujumbe huo na kumuhakikishia kua Tanzania itaendelea kua rafiki na ndungu wa dhati wa Burundi.

Kuhusu hali ya Burundi, Rais magufuli alisema kama anaamini kua wasuluhishi mgogoro wa Nchi hiyo: Rais Yoweri Museven wa Uganda, Rais mtaafu wa Awamu ya Tatu, na Benjamin Mkapa watafanikiwa kuusuluhisha.

 

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *