Mahojiano Na shaddy Mtumishi

By  |  0 Comments

Kwa wengi ni mtayarshaji video shupavu ,kwa wengine  ni mwanamziki anayeibuka kwa kasi .Kutana Na mwanamziki Shadrack  Mwongela  maarufu kama shaddy  Mtumishi mwanasanaa anaye ngaa nchini Kenya .


 Kwa faida ya wasomaji wetu Shaddy Mtumishi ni Nani ?

Shaddy Mtumishi ni mwandishi na Muimbaji wa nyimbo za injili, mwelekezi wa filamu (Mshindi wa tuzo za Xtreem 2016 na 2017) na zaidi ya yote ni kijana aliyeokoka.
 Ni lini Na nini kilikuchochea ujiunge Na tasnia ya mziki?

 Nimefanya mziki kwa mda kidogo ila rasmi itakuwa ni mwaka huu wa 2018. Hakuna kilicho nivutia kufanya mziki kwa maana mziki Umekuwa ndani yangu tangu jadi. Nilijipata tu nikipenda mziki kwa sana… naeza sema nikama ulikuwa tu kwa damu
 Safiri yako kwa mziki waweza sema imekuwa aje  ?

Haijakuwa laini vile, changamoto kibao za kuanzia na kujifunza mengi lakini kwa yote na mshukuru Mola.

Ukitaja kwamba safari ya mziki imekuwa Na changamoto ,ni changamoto zipi umekumbana nazo ?

Ni kadhaa zikiwemo, kuskuma mziki kwa vyombo vya habari Ili uweze kuwafikiwa wengi, pia gharama ya za studio na kufanya video nzuri nzuri.

Mwaka huu Na mwaka Jana ulifanya‘ cover ‘ya wimbo wake Good luck Gozbert shukrani Na ile yake Joel Lwanga sitabaki nilivyo tujuze zaidi kuzihusu?

 Shukurani ni wimbo ambao ulibariki nasfi yangu kwa sana hadi nikaupenda. Nlikuwa najipata mara nyingi nikiuskiza tu wimbo wenyewe mara nyingi kwa Siku ndo baadae nikenda studio kuufanyia kazi. Sitabaki nilivyo, pia ni wimbo wenye kutia moyo sana na uzito wa ujumbe wake ndo ulinipelekea kuufanyia cover

Mbali Na uimbaji wewe ni mtayarshaji video nchini Kenya haswa zile za injili ?

 Naam,Shaddy Mtumishi ni mtayarishaji wa video za injili.Ndo kazi rasmi ninayo ifanya mbali na mziki.

Umeishughulikia video zipi ?

 Ni nyingi zikiwemo za David Kasika, Tumaini, Solomon Mukubwa, Ali Mukwana, Mtaliano Eliano, Burton King na kadhalika

 Ni mafunzo yepi umepata kutokana  Na kuwa mtayarshaji video Na pia muuimbaji

Nimejifunza uvumilivu na unyenyekevu… Katika uimbaji lazima ujue kila mtu ana wakati wake lakini cha msingi zaidi ni kungojea wakati wa Mungu

https://youtu.be/r40Rd6XAOHo

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *