Kenya Wild Life: Simba ”wapenzi wa jinsia moja” wapigwa picha Kenya

By  |  0 Comments

Picha moja ya simba wawili wa kiume walioonekana katika mbuga moja ya wanyama nchini Kenya wakifanya tendo la ngono imezuia hisia kali nchini humo. 

Tayari afisa wa bodi simamizi ya udhibiti wa filamu Kenya anasema kuwa wanyama hao huenda wamejifunza tabia hiyo kutoka kwa binadamu.
”Wanyama hawa wanahitaji kupitia ushauri nasaha kwa sababu huenda wamejifunza tabia hii kwa wapenzi wa jinsia moja wanaozuru mbuga hizo na kufanya tabia mbaya”’, aliseama Ezekiel Mutua , ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa bodi ya kukagua viwango vya filamu nchini Kenya KFCB.
Matamshi ya Mutua yanajri baada ya picha zilizopigwa na mpiga picha wa Uingereza Paul Goldstein kuonyesha simba wawili wa kiume wakielekea katika kichaka katika mbuga ya Masai Mara iliopo kusini magharibi mwa Kenya .

Share Button

Share Button

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *