Kenya John Kiarie – Tumeanza kipindi chetu kwa Shillingi Hamsini
Mbunge wa Dagoretti kusini John kiarie ambaye pia alikuwa mchekeshaji wa kipindi cha redykyulass amewashangaza wengi, mbunge huyu ambaye anafahamika kwa jina lake LA steji KJ amedai kuwa kipindi cha redykyulass kilianza na shillingi hamsini ambayo ilitumika kama nauli ya wachekeshaji waanzilishi Nyambane, kj na Tonny Njuguna kuenda show yao ya kwanza.
kipindi hicho kilikuwa kinaangazia maswali ya ukombozi wa nchi ya kenya ( liberation ) kupitia uchekesaji na uigaji wa tabia ya viongozi japo wengi waliichukulia kama kejeli kwa wanasiasa ile hawakujua ni kuwa mbali na Redykyulass kuibua wachekesaji wanaonziwa kama Daniel Ndambuki( Churchill) kipindi cha redykyulass iliwahamashisha wakenya kuhusu siasa za nchi .wachekesaji hawa waanziliahi bado wanapewa heshima kwa ujasiri waliyokuwa nayo japo Uhuru wa kujieleza haukuwa ukikumbatiwa ” tulianza kipindi yetu Redykyulass kwa shillingi hamsini kila mmoja ambayo ilikuwa nauli.kuli wengi hawajui nikuwa mikakati ndio inaleta fedha sio fedha inaleta fedha.”
Article by Erick Mutinda